Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. GIBSON B. MEISEYEKI aliuliza:- Mheshimiwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliahidi ujenzi wa barabara yenye urefu kwa kilomita 12 katika Jimbo la Arumeru Magharibi na sasa imepita miaka 10 bila kutekelezwa ahadi hiyo:- Je, ni lini sasa Serikali itatekeleza ahadi hiyo hasa ikitiliwa maanani kuwa katika Jimbo la Arumeru Magharibi hakuna barabara ya lami hata nusu kilomita?

Supplementary Question 1

MHE. GIBSON B. OLE MEISEYEKI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nimekuwa nikisubiria majibu ya swali hili kwa miaka mitatu sasa, lakini majibu niliyopewa siyo ya barabara ambazo Mheshimiwa Rais aliziahidi. Rais alipokuwa anaomba kura mwaka 2005 alitoa ahadi ya kilomita 12 ya bararaba inayoanzia Ngaramtoni kupitia hospitali ya Selian mpaka kwa Luhiyo kilomita 12. Alipochaguliwa 2012 akatuongeza barabara nyingine inayokwenda Hospitali ya Oltrumeti. Barabara zote hizi hazina lami mpaka sasa. Je, ni lini sasa Serikali itapata fedha ili iweze kuteleza ahadi hiyo ya Rais kwa barabara hizo ambazo alituahidi hizi nyingine alizozisema Mheshimiwa Waziri hazihusiani na swali langu?

Mheshimiwa Spika, pia ametaja kwamba barabara ya Sarawani inatengenezwa, ni kweli, lakini imekuwa ikitengenezwa kilomita 0.8 kwa takriban mwaka mzima sasa haijakamilika. Je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari kuongoza na mimi kwenda Arumeru Magharibi tukaangalie maendeleo na ubora wa barabara hii ya Sarawani - Oldonyosapuk ambayo kwa zaidi ya mwaka mzima inatengenezwa na bado haijakamilika?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, nilikuwa na wasiwasi kwamba Mheshimiwa Mbunge angesema barabara hizi hazijaja kwenye jimbo lake lakini na yeye tunakubaliana kwamba barabara hizi zimejengwa kwenye jimbo lake, kwa hiyo, naamini kuwa Mheshimiwa Mbunge ana kila sababu ya kuipongeza Serikali kwa kujenga barabara hizo ndani ya jimbo lake.

Mheshimiwa Spika, lakini naomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba ahadi ambazo tumetoa ni ahadi thabiti na kwa kadri uhitaji wa wakati unavyoruhusu ndio tunaenda kwenye barabara hizo. Kwa hiyo naomba nimhakikishie kwamba ahadi za Rais wetu aliyetangulia ambaye sasa amepokea kijiti Rais tuliyenayo bado ni ahadi za CCM, tutazitekeleza kwa kadiri bajeti itakavyoruhusu.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge anaomba fursa nikatazame hiyo barabara ambayo imekuwa ikitengenezwa ya kilomita 0.8, nalo ni jambo la kushukuru kwa sababu angeniambia kuwa haijaanza kutengenezwa kabisa then hata kuongea kwake ingekuwa tofauti. Naomba nimhakikishie kwa kadiri ratiba itakavyokuwa inaruhusu mimi nipo tayari kuambatana naye.