Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Primary Question

MHE. JUMA OTHMAN HIJA aliuliza:- Mradi wa kupeleka Umeme Vijijini (REA) ni mradi ambao unaendelea kwa kasi kubwa nchi nzima. Je, Serikali inaweza kutuambia ni kwa kiasi gani umeme huu umesambazwa nchi nzima (coverage) tangu mradi huu ulipoanza?

Supplementary Question 1

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwanza na mimi nipongeze Wizara kwa speed nzuri wanayochukua ya kusambaza umeme vijijini. Hata hivyo nina suala moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maeneo ambayo Mheshimiwa Wazairi ametueleza pia kuna taasisi za Serikali ambazo Mheshimiwa Waziri hakuzitaja. Je, nini mikakati ya kuziunganishia taasisi za Serikali, umeme?

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Hija kwa pongezi zake kwenye swali lake; la nyongeza ameuliza mkakati wa Serikali wakusambazia umeme taasisi za Kiserikali. Kama nilivyosema kwenye jibu langu la mzingi katika utekelezaji wa REA I na II kulikuwa na mapungufu ya kuruka baadhi ya maeneo na hususani Taasisi za Kiserikali utekelezaji wa REA III kama Serikali tumetoa maelekezo kwamba taasisi zote za Serikali zipatiwe kipaumbele na napenda kuwashukuru wakandarasi wote wamekuwa wakitekeleza maelekezo haya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo napenda nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwa sasa kwa makandarasi wameendelea kuunganisha maeneo ya Kiserikali iwe ya zahanati, miradi ya maji, vituo vya afya na hospitali. Nakushukuru.