Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prof. Norman Adamson Sigalla King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. PROF. NORMAN S. KING aliuliza:- Hifadhi ya Kitulo iliyoko Mkoa wa Njombe, Wilaya ya Makete ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu na ni hifadhi ya kipekee katika Afrika kwa sababu ina aina tofauti ya maua zaidi ya 120. Je, ni lini TANAPA kwa kushirikiana na TANROADS itaona umuhimu wa kujenga kwa lami barabara ya kutoka Chimala – Matamba – Kitulo – Makete ili kurahisisha uingiaji wa watalii kwenye mbuga hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. PROF. NORMAN S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha kidogo kwa sababu, kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ukurasa wa 51 iko bayana, barabara hii imetajwa kwamba ni muhimnu iwekwe kiwango cha lami. Ni lini Serikali itapeleka nguvu kuhakikisha kwamba hili linatekelezwa ili kuboresha miundombinu hii?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mwaka 2017 Serikali ilikuwa imeahidi kupeleka wanyama kwenye hifadhi hii ili kuongeza vivutio kwenye Hifadhi ya Kitulo. Ni lini mpango wa kupeleka wanyama wasio wakali, ukiacha simba, kwenye hifadhi hii utakamilika?

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijajibu maswali hayo naomba nichukue nafasi hii kwanza kumpongeza kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya, lakini pia nimpongeze kwa jitihada kwamba sasa hivi anaenda kuoa na amesambaza kadi. Kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wabunge wamchangie ili akamilike, aendelee kufanya kazi vizuri. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa hii barabara iko katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwamba itajengwa kwa kiwango cha lami, lakini naomba nimjulishe Mheshimiwa Mbunge tu kwamba hivi sasa barabara ambayo inawekwa lami ni ile ambayo inatoka Njombe hadi Makete, inawekwa lami sasa hivi na bado kuna barabara nyingine ya kutoka Isonje – Makete mpaka Mbeya, nayo iko kwenye feasibility study. Hii barabara ya tatu itakuja kuunganishwa na hizi barabara nyingine mbili ambazo nimezisema na ninaamini kabisa hali itakuwa ni nzuri na Mheshimiwa Mbunge utafurahia baada ya hilo suala kukamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuhusu ni lini wanyama wale ambao tuliahidi kwamba tutawapeleka katika Hifadhi yetu ya Kitulo, Serikali ina mpango wa kupeleka wanyama 25. Ili kuhamisha wanyama kutoka hifadhi moja kwenda hifadhi nyingine kuna taratibu za kisheria ambazo ni lazima zikamilike. Hivi sasa zimeshakamilika na Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii amesharidhia wanyama 25 wahamishiwe katika Hifadhi yetu ya Kitulo kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge naamini baada ya muda mfupi utawaona hao wanyama.