Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Primary Question

MHE. RIDHIWANI J. KIKWETE aliuliza:- Maeneo mengi ya Halmashauri ya Chalinze yamefaidika na Mradi wa REA Awamu ya Pili lakini katika utekelezaji wa mradi huo Miji ya Kiwangwa, Hondogo, Mkange na Kibindu bado haijafikiwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuifikia miji hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. RIDHIWANI J. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini mahitaji ya umeme katika maeneo mengi hasa katika Vitongoji vya Halmashauri ya Jimbo la Chalinze imekuwa ni muhimu sana. Kwa mfano, kule Msinune, Kiwangwa bado umeme haujafika na ahadi ya Serikali ni kwamba umeme hautaruka Kitongoji chochote.
Je, Serikali imejipangaje katika kuhakikisha kwamba inawapelekea umeme wananchi wanaoishi katika vitongoji hivyo vikiwemo vile ambavyo vipo katika Kata ya Vigwaza na Mbwewe na maeneo mengine ya Halmashauri yetu? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza nami niwe mmoja wa kumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa Mbunge wetu wa Chalinze, Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Mheshimiwa Ridhiwani atakumbuka kwamba mwezi wa Kumi na Mbili tulifanya ziara pamoja naye na Waheshimiwa Wabunge wengine wa Mkoa wa Pwani kwenye majimbo yao; tulipita katika maeneo ya Kata ya Kiwangwa, Msinune na Bago na Mheshimiwa Mbunge atakumbuka pia tuna mradi wa densification unaoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Chalinze.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, maeneo ambayo ameyataja ya Msinune na Bago ni maeneo ambayo yapo katika mradi wa REA Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza. Kwa hiyo, nimthibitishie Mhesimiwa Mbunge Serikali ya Awamu ya Tano kwa kweli kupitia miradi yake hii inayoendelea itapeleka umeme katika vitongoji mbalimbali ambavyo vina changamoto.
Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana kwa kazi yake ya kufuatilia hasa upatikanaji wa nishati ya umeme Jimboni Chalinze. Ahsante. (Makofi)