Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:- Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua kama Serikali ya viwanda na kuna Shirika la Serikali lililoanzishwa kwa ajili ya kuanzisha na kuimarisha Viwanda Vidogo Vidogo vya SIDO . (a) Je, kwa kiasi gani Serikali imeliwezesha Shirika hilo katika kufikia malengo yake na malengo ya Serikali kwa Tanzania ya viwanda? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kuwa Shirika hilo linakuwa na matawi katika kila Wilaya tofauti na sasa kuwa na Ofisi katika ngazi za Mikoa tu?

Supplementary Question 1

MHE. CECILIA DANIEL PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kumekuwa na Mamlaka nyingi za usimamizi na uwezeshaji katika mipango ya Serikali hasa katika suala hili la la viwanda.
(a) Je, Serikali kupitia SIDO ina mkakati gani wa kuunganisha mipango hii na hiyo mipango ikaunganishwa na rasilimali watu wanaozalishwa katika vyuo vyetu vya Ufundi hapa nchini?
(b) Sera na usimamizi wa kodi ni mambo muhimu sana katika kufanikisha suala la viwanda. Je, ulipwaji na utozwaji wa kodi unaofanywa na mamlaka husika hapa nchini, umezingatia vipi suala hili ili kutokuhathiri sekta hii changa ambayo inakua?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, niseme tu kwamba katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ni kwamba suala hili ni mtambuka na linafanywa na wadau mbalimbali na sekta nyingi na hivyo hata usimamizi ulikuwa umepangwa zaidi kulingana na uhalisia wa eneo ambao usimamizi wake unahitajika ufanyike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano kwenye suala la madawa na vyakula, tunazungumzia masuala ya kiafya. Kwa hiyo, unaangalia kwamba kulikuwa na kuangalia mamlaka hiyo ya usimamizi itakuwa imeweza kufanya kazi zake vizuri na kuondoa vikwazo kwa kiasi gani kama itakuwa imekaa katika eneo hilo. Hata hivyo, Serikali imekuwa ikiendelea kufanyia kazi suala hilo ili kuona namna bora zaidi ya hizi mamlaka za usimamizi zinavyoweza kuunganishwa ili kuweza kuleta tija zaidi katika uchumi huu wa maendeleo ya viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, halikadhalika, kwa suala ambalo ni la SIDO kuwa yeye sasa kama muunganishaji. Kimsingi SIDO haifanyi kazi peke yake, mfano tu kwamba kwa mfano katika Mkoa wako wa Manyara ukiangalia katika suala la uendelezaji wa zao la vitunguu swaumu, pale tayari kuna wadau wengi ambao wamehusika MIVAP ambao kulikuwa na jengo pale lakini pia katika chain ya kuongeza thamani, ukienda Magugu kuna SNV wanaoshirikiana na SIDO katika uongezaji thamani katika eneo la mpunga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, halikadhalika na katika eneo la Hanang, vilevile kuna suala la kuangalia menejimenti ya kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna. Kwa hiyo, kimsingi ni kwamba lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba wadau wote wanaunganika pamoja na kila mtu kuweka intervention katika eneo linalohusika ili kuweza kupata tija katika uendelezaji wa wajasiriamali na viwanda kwa ujumla.