Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Eng. Joel Makanyaga Mwaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chilonwa

Primary Question

MHE. JOEL M. MAKANYAGA aliuliza:- Serikali ilikuja na mpango mzuri wa umeme Vijijini na kupitia mradi wa REA kukawa na REA I, REA II na sasa REA III na Serikali iliahidi kwamba miradi yote ya REA II ambayo haijakamilika hadi kuanzishwa kwa REA III itatekelezwa sambamba na REA III:- (a) Je, ni lini Serikali itatekeleza miradi yote ya REA II Jimbo la Chilonwa katika Vijiji vinne vya Kata ya Msamalo(Myunga, Msamelo, Mnase na Mlebe) Vijiji viwili vya Kata ya Zajilwa (Zajilwa na Mayungu) na Kijiji cha Kata ya Manchali? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuviingiza vijiji ambavyo havikuwepo kwenye mpango wa REA II katika mpango wa REA III?

Supplementary Question 1

MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Naibu Spika ahsante. Naishukuru Serikali kwa majibu mazuri na naamini kwamba haya yaliyozungumzwa yote yataenda kutekelezwa. Naomba kuongeza swali moja la nyongeza.
Kwa kuwa, Vijiji vingi vya Jimbo langu ni vikubwa sana na kwa kuwa, umeme huu wa REA umekuwa ukifikishwa kwenye maeneo ya kati ya vijiji tu. Je, Serikali haioni kwamba kuna haja ya kuusogeza umeme huu sasa kwenye vitongoji vilivyo mbali na maeneo ya kati ya vijiji ili wananchi hao katika vitongoji hivyo nao waweze kunufaika na umeme huu?
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza katika jibu langu la msingi, namshukuru sana Mheshimiwa Makanyaga kwanza kwa kuuliza swali hili.
Kwa kuwakumbusha tu, ni kweli kabisa kwa awamu ya II tumepeleka kwenye vituo, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Chilonwa kwamba awamu ya III inapeleka sasa kwenye vitongoji na kwenye vijiji vyote na kwenye mashine na kwenye taasisi za jamii ikiwemo shule. Nimhakikishie hata Kijiji chake Mheshimiwa Chilonwa cha Chalinze sasa kitapata umeme, Kijiji chake cha Kawawa kitapata umeme, Kijiji cha Malichela kitapata umeme, Kijiji cha Membe kitapata umeme, Kijiji cha Bwawani nacho kitapata umeme. Kwa hiyo, nimhakikishie kuwa vijiji vyote vitapata umeme.

Name

Lathifah Hassan Chande

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOEL M. MAKANYAGA aliuliza:- Serikali ilikuja na mpango mzuri wa umeme Vijijini na kupitia mradi wa REA kukawa na REA I, REA II na sasa REA III na Serikali iliahidi kwamba miradi yote ya REA II ambayo haijakamilika hadi kuanzishwa kwa REA III itatekelezwa sambamba na REA III:- (a) Je, ni lini Serikali itatekeleza miradi yote ya REA II Jimbo la Chilonwa katika Vijiji vinne vya Kata ya Msamalo(Myunga, Msamelo, Mnase na Mlebe) Vijiji viwili vya Kata ya Zajilwa (Zajilwa na Mayungu) na Kijiji cha Kata ya Manchali? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuviingiza vijiji ambavyo havikuwepo kwenye mpango wa REA II katika mpango wa REA III?

Supplementary Question 2

MHE. LATHIFAH H. CHANDE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, mpango huu wa REA upo kwa ajili pia ya Mkoa wa Lindi hadi Lindi Vijijini, lakini mpaka sasa hivi maeneo mengi ya Mkoa wa Lindi bado hayana umeme. Je, ni vijiji vingapi katika Mkoa wa Lindi ambavyo vinatarajia kupewa umeme wa REA katika bajeti ya mwaka 2016/2017?

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, Vijiji vinavyotarajiwa kuunganishwa umeme katika Mkoa wa Lindi kupitia REA Awamu ya III ni 117. Ahsante sana.

Name

Mariamu Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOEL M. MAKANYAGA aliuliza:- Serikali ilikuja na mpango mzuri wa umeme Vijijini na kupitia mradi wa REA kukawa na REA I, REA II na sasa REA III na Serikali iliahidi kwamba miradi yote ya REA II ambayo haijakamilika hadi kuanzishwa kwa REA III itatekelezwa sambamba na REA III:- (a) Je, ni lini Serikali itatekeleza miradi yote ya REA II Jimbo la Chilonwa katika Vijiji vinne vya Kata ya Msamalo(Myunga, Msamelo, Mnase na Mlebe) Vijiji viwili vya Kata ya Zajilwa (Zajilwa na Mayungu) na Kijiji cha Kata ya Manchali? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuviingiza vijiji ambavyo havikuwepo kwenye mpango wa REA II katika mpango wa REA III?

Supplementary Question 3

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuuliza swali la nyongeza. Katika Mkoa wa Dar es Salaam bado kuna maeneo mbalimbali katika Kata ya Mianzini maeneo ya Mponda Wilaya ya Temeke, Chamanzi, Tuangoma, Somangila, Kimbiji, Pemba Mnazi, Vijibweni, Chanika, Majohe na Pugu, vyote hivyo bado havijapata miradi ya umeme kusambazwa katika vijiji mbalimbali.
Je, Mheshimiwa Waziri, ni lini sasa Serikali itasambaza umeme pembezoni mwa vijiji hivi vya Mkoa wa Dar es Salaam?

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa maeneo ya Dar es Salaam maeneo mengi hatujapeleka umeme na hasa Kigamboni. Awamu ya kwanza tunayofanya tunapanga kujenga sub-station Kigamboni kwa sababu population ya sasa ni kubwa. Kwa hiyo, vitongoji vyote vya Kigamboni vitapelekewa umeme kupitia Awamu ya II. Pia maeneo ya Chanika, maeneo ya Gongo la Mboto, maeneo ya Kinyamwezi, maeneo ya Buyuni na yenyewe yanapelekewa kwenye mpango huu wa REA unaoanza mwezi Desemba.