Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Primary Question

MHE. DEO K. SANGA aliuliza:- Kutoka Kijiji cha Mutelewele kwenda Makambako ni kilometa tano wakati kwenda Halmashauri ya Wanging‘ombe ni kilometa 65; kutoka Kata ya Soja kuja Makambako Mjini ni kilometa 25 na kwenda Halmashauri yao ya Wanging‘ombe ni kilometa 88 na kutoka Kijiji cha Nyigo kuja Makambako ni kilometa 8 wakati kwenda Halmashauri ya Mufindi ni kilometa 88 na huduma zote zikiwemo matibabu wanazipata Makambako; kutoka Kijiji cha Igongolo ni umbali wa kilometa 6 kwenda Makambako wakati kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ni kilometa 54. (a) Je, Serikali itakuwa tayari kugawa mipaka upya ili wananchi wapate huduma karibu na Halmashauri yao ili iendane na kauli mbiu ya kusogeza huduma karibu na wananchi? (b) Je, ni lini sasa Serikali itapima upya mipaka hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri lakini naomba niulize maswali ya nyongeza mawili kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu swali langu la msingi nimeelezea namna ambavyo wananchi wa Kata ya Saja, Kijiji cha Nyigo na Mtewele namna wanavyopata tabu kwani huduma zote zinapatikana Makambako na kwenda kwenye Halmashauri yao kutoka Saja kwenda Wanging‘ombe ni kilometa 88 na kwenda Makambako ni kilometa 20 na kutoka Mtewele ni kilometa tano na Waziri amekiri ni kweli katika suala la upatikanaji wa huduma ni mbali. Kwa nini Waziri asiagize shughuli hii ya vikao ianze kufanyika? Siku za nyuma vilishafanyika na kupelekwa kwenye vikao vinavyohusika vya mkoa na hivi juzi tu tulikaa kwenye kikao na mkoa tayari walianza kushughulikia. Niombe Waziri sasa ashughulikie suala hili na kuagiza kwamba waweze kukaa vikao ili wananchi hawa wapate huduma jirani.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika Kijiji cha Nyigo, GN ambayo iko katika Halmashauri ya Makambako inaonyesha Kijiji cha Ngigo mpaka wake mwisho ni barabara ya zamani ya Mgololo. Hata hivyo, uongozi wa Iringa umewahi kwenda pale na kutaka kupotosha ukweli. Niombe sasa Waziri asimamie na afuatane na mimi ili tukaone ile GN ambayo tulipewa Halmashauri ya Mji wa Makambako ili wananchi wale waweze kupata huduma jirani na Mji wa Makambako. Nakushukuru.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna suala zito kama linalohusu mipaka. Mimi namuelewa sana Mheshimiwa Sanga katika concern yake hiyo, wananchi wanahitaji kweli kwenda eneo hilo lakini kwa sababu maeneo ya mipaka yameshaainishwa itakuwa ni vigumu leo niagize kufanya jambo fulani. Isipokuwa nifanye jambo moja, endapo haya mahitaji yanaonekana ni ya msingi, kama nilivyosema katika jibu langu la awali, Mheshimiwa Deo Sanga najua una ushawishi mzuri sana katika maeneo yale na ukizingatia kwamba ulikuwa Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa kwa hiyo kauli yako inasikika vizuri sana, nadhani mchakato ukianza kama nilivyoeleza katika vikao vyetu vya vijiji vya WDC, DCC na RCC jambo hili litaisha vizuri. Jambo hili linaenda hadi kubadilisha zile coordinates katika GN, ndiyo maana nasema lazima liwe shirikishi, watu wa maeneo hayo wakubaliane kwa pamoja ni jinsi gani tutafanya kama tunataka kubadilisha mipaka. Kwa mujibu wa Sheria Sura 287, kifungu cha 10 mpaka 11 vimempa mamlaka Waziri mwenye dhamana kubadilisha mipaka lakini ni endapo itaonekana ninyi mmemaliza mchakato huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la Kijiji cha Nyigo kwamba GN zimebadilishwa yaani haziko sawasawa, naomba niseme kwamba katika hilo niko radhi kutembelea kijiji hicho. Katika safari zangu za Nyanda ya Juu Kusini nitamshirikisha na nitamuomba tushirikiane kama tulivyoshirikiana katika ziara yangu iliyopita lengo kubwa likiwa ni kuleta mtengamano mzuri katika maeneo yetu.

Name

Stanslaus Shing'oma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. DEO K. SANGA aliuliza:- Kutoka Kijiji cha Mutelewele kwenda Makambako ni kilometa tano wakati kwenda Halmashauri ya Wanging‘ombe ni kilometa 65; kutoka Kata ya Soja kuja Makambako Mjini ni kilometa 25 na kwenda Halmashauri yao ya Wanging‘ombe ni kilometa 88 na kutoka Kijiji cha Nyigo kuja Makambako ni kilometa 8 wakati kwenda Halmashauri ya Mufindi ni kilometa 88 na huduma zote zikiwemo matibabu wanazipata Makambako; kutoka Kijiji cha Igongolo ni umbali wa kilometa 6 kwenda Makambako wakati kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ni kilometa 54. (a) Je, Serikali itakuwa tayari kugawa mipaka upya ili wananchi wapate huduma karibu na Halmashauri yao ili iendane na kauli mbiu ya kusogeza huduma karibu na wananchi? (b) Je, ni lini sasa Serikali itapima upya mipaka hiyo?

Supplementary Question 2

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na nishukuru pia kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri.
Mheshimiwa Naibu Spika, matatizo yaliyoko kwenye Jimbo la Makambako yanafanana sana na matatizo yaliyoko kwenye Jimbo la Nyamagana katika Kata za Kishiri na Igoma. Majibu ya Mheshimiwa Waziri ni mazuri sana ila nilitaka tu kupata uhakika kutoka kwake na sisi ambao tuna matatizo ya kupata huduma kati ya Kata ya Kishiri na Igoma tukirudia mchakato huu upya kuanzia kwenye ngazi zote ambazo amezitaja tukaleta kwake tutapata approval ya kufanya marekebisho kwa wakati? Nashukuru.

Name

George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri Jafo, napenda niongezee kwenye swali la nyongeza lililoulizwa na Mheshimiwa Mabula kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kumekuwa na migogoro mingi ya mipaka ambayo kimsingi si yote inaitwa migogoro. Wakati mwingine kulitokea makosa wakati wa kutafakari mipaka hiyo na kugawanya mamlaka za utawala lakini wakati mwingine inatokana tu na mabadiliko ya kijiografia na mahitaji yameelekea upande ambao pengine busara sasa inataka namna mpya itizamwe ili kuweza kurekebisha mipaka hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu niwashauri Waheshimiwa Wabunge kwamba michakato hii kwa mfumo wa kisheria na taratibu zake inaanzia huko huko chini. Kama ninyi huko chini mtatoa kwenye vikao vyote vya Wilaya na Mkoa mkawa mmekubaliana sisi huku kubadilisha hizi GN si tatizo kubwa. Kwa hiyo, niwaombe sana Waheshimiwa Wabunge mkazitaarifu mamlaka na vikao vinavyohusika viweze kufuata taratibu za kisheria kama zinavyotaka na kama walivyopendekeza mpaka tukafikia kuweka mipaka hiyo, wafanye hivyo hivyo katika kupendekeza kama wanataka kubadilisha mipaka hiyo na sisi Serikali hatutakuwa na pingamizi katika jambo hilo.