Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. CHARLES M. KAJEGE aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga Malambo ya kunyweshea mifugo katika Jimbo la Mwibara?

Supplementary Question 1

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza na naishukuru Serikali kwa kuchimba Bwawa la Kihumbu. Sasa nataka kuuliza, kwa sababu bwawa limechukua muda mrefu kidogo pamoja na kwamba jitihada zipo.

Je, ni lini sasa hilo bwawa litakamilika ili wananchi watumie maji ya bwawa hilo na mifugo?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli bwawa halijakamilika; Serikali tayari imeshakutana na mkandarasi na imeshampa deadline juu ya lini bwawa linatakiwa kukamilika na tayari tumeshakubaliana. Mara tu mkataba utakapokuwa umekamilika bwawa hilo litakuwa limekamilika na atatukabidhi Serikallini kwa ajili ya kuendelea kulitumia.