Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha mchakato wa kuanzisha Halmashauri ya Wilaya ya Sumve ili kusogeza huduma kwa wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Busokelo ukizingatia mpaka sasa ni miaka 10 imepita? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala katika halmashauri zetu. Nawapongeza Halmashauri ya Busokelo kwa kupokea fedha za Serikali Kuu, lakini jengo halijakamilika kama Mheshimiwa Mbunge anavyosema. Naomba nilichukue hilo nilifanyie kazi tuweze kuona kiasi gani cha fedha hakijapelekwa kwa ajili ya ukamilishaji na tuweze kuweka mpango kazi kuhakikisha kwamba sasa fedha hiyo inapatikana lakini jengo hilo linakamilishwa kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Busokelo, ahsante.