Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuomba fedha katika mifuko ya kupunguza hewa ukaa duniani na kuwalipa wananchi wanaopanda na kutunza misitu katika Wilaya ya Kilolo?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri; je, Serikali ina mpango gani wa kuwatumia vijana waliohitimu masomo ya environmental science katika kusaidia kueneza elimu hii ya kupunguza hii hewa ya ukaa?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI. OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la mama yangu, Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara kutoka Mkoa ule wa Ruvuma, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli sasa hivi tuna vijana wengi sana wamehitimu environmental science katika vyuo mbalimbali ikiwepo Dar es Salaam, SUA pamoja na University of Dodoma na vyuo vingine.

Mheshimiwa Spika, na ndiyo maana katika ajenga hiyo kikubwa zaidi tunachokifanya ni kwamba si rahisi Serikali ikaajiri watu wote, lakini tumeweka suala zima la kuleta hamasa katika makundi mbalimbali hasa kutumia vijana hawa na hasa wakati fulani nilipokuwa katika mkutano pale Dar es Salaam, mkutano unaohusiana na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi tulitoa maelekezo katika NGOs mbalimbali sasa zifungue milango kwa vijana waliosoma environment science. Hata kuwapa internship au mikataba ya muda mfupi kwa lengo kubwa vijana hawa waweze kutumia kiupana zaidi kwa ajili ya Taifa letu hili.

Mheshimiwa Spika, imani yangu maelekezo yale tuliyoyatoa katika taasisi mbalimbali wenzetu wataenda kuyazingatia kwa lengo kubwa vijana hawa waweze kutumika kwa mustakabali wa nchi yetu katika utunzaji wa mazingira.

Name

Asya Mwadini Mohammed

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuomba fedha katika mifuko ya kupunguza hewa ukaa duniani na kuwalipa wananchi wanaopanda na kutunza misitu katika Wilaya ya Kilolo?

Supplementary Question 2

MHE. ASYA MWADINI MOHAMMED: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi; kwa kuwa utunzaji wa misitu iwe ya mikoko ama ya kawaida husaidia sana katika utunzaji wa mazingira.

Swali langu kwa Serikali; je, Serikali ina mpango gani wa kuvitambua vikundi vyote vinavyojitolea kwa maksudi katika utunzaji wa mikoko hasa kwa upande wa Zanzibar?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la dada yangu Asya, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Zanzibar, kama ifuatavyo:-

Kwanza nipongeze vikundi vyote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bara na Visiwani wanajihusisha katika ajenda ya mazingira jambo hilo ni jambo jema sana na sisi kama Serikali jukumu letu kubwa ni kuwatambua. Lakini si kuwatambua peke yake, juzi juzi tulikuwa na mkutano kule Belgium katika miradi maalum inayosemwa miradi ya hewa ukaa na miongoni mwa ajenda kubwa jinsi gani vikundi hivi vidogo vidogo vinavyochipua katika ajenda ya mazingira baadaye vifanyiwe utaratibu maalum wa uwezeshaji kwa ajili ya ajenda ya kulinda mazingira, lakini ajenda ya kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo jambo hilo ni jukumu letu Ofisi ya Makamu wa Rais tutaendelea kulifanya na kama mnavyoona bajeti yetu iliyopita imelenga vilevile katika suala zima la capacity building katika makundi na vikundi mbalimbali hilo ni jukumu letu tutaenda kulifanya kwa upana mkubwa zaidi ikiwemo Zanzibar. Ahsante sana.

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuomba fedha katika mifuko ya kupunguza hewa ukaa duniani na kuwalipa wananchi wanaopanda na kutunza misitu katika Wilaya ya Kilolo?

Supplementary Question 3

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru; katika Kata ya Kimara na Kata ya Idete yupo mwekezaji ambaye ni Kampuni inaitwa Odzungwa Corridor na yeye anafanyakazi ya kupanda miti kwa ajili kuja kuvuna hewa ya ukaa miaka ijayo.

Sasa je, Serikali haioni umuhimu wa kuzungumza naye ili aweze pia kushirikisha misitu iliyopo tayari ili huo uvunaji uweze kuanza na malipo yaweze kufanywa kwa sababu ipo miti ambayo iko tayari?

Lakini swali la pili; moja kati ya lengo la kuwepo kwa misitu kimsingi ni hifadhi ya mazingira na hivi karibuni bei za mazao ya misitu hususan mbao imeshuka sana na kama inakatisha tamaa wakulima kuendelea kulima miti na baadaye tutapata madhara makubwa.

Ni nini kauli ya Serikali kuhusu tatizo hili ambalo linaweza likawa na matatizo makubwa baadaye? Ahsante.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI. OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la ndugu yangu, Mheshimiwa Justin Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo:-

Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa sababu kwa mara kadhaa alikuwa akizungumzia hoja ya upandaji wa miti wa kibiashara hususan katika wilaya yake ya Kilolo na Mkoa mzima wa Iringa pamoja na Mkoa wa Njombe wanavyojihusisha na upandaji wa miti.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ajenda ya huyu mkulima ambayo analima hii miti ni kama tunavyosema kwamba tumeandaa mwongozo sasa, mwongozo huu uta-address suala zima la uhifadhi wa mazingira na watu mmoja mmoja mara baada ya mwongozo huu watapewa maelekezo jinsi gani ya kushiriki vyema kwa ajili ya kupata utajiri mkubwa kupitia suala la misitu. Kwa hiyo, afanye subira tu nadhani kwa malengo yake yanaendana pamoja na mkakati wa Serikali tunaoendelea nao.

Mheshimiwa Spika, lakini suala zima misitu, thamani ya miti inashuka, basi niseme kwamba katika hilo kwetu sisi upande wa Mazingira tuseme kwamba hiyo ni fursa sasa kwa wale ambao wanaopanda miti ambao kesho na keshokutwa biashara hii hewa ya ukaa itapokuwa kubwa tutaenda kufanya mambo mawili; kwanza kutunza mazingira, lakini jambo la pili vilevile kuhakikisha kwamba tunakabiliana na mabadiliko ya tabianchi lakini kikubwa zaidi kuhakikisha tunapeleka utajiri wa mtu mmoja mmoja kupitia ajira ya misitu, ahsante.

Name

Ramadhan Suleiman Ramadhan

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuomba fedha katika mifuko ya kupunguza hewa ukaa duniani na kuwalipa wananchi wanaopanda na kutunza misitu katika Wilaya ya Kilolo?

Supplementary Question 4

MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza; kwenye majibu yake Mheshimiwa Waziri amekiri kwamba wapo kuandaa mwongozo utakaoruhusu wawekezaji kuja kuwekeza kwenye kupunguza makali ya hewa ya ukaa; ni lini mwongozo huo utakamilika?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI. OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, ni kwamba kwanza nimshukuru Mheshimiwa Ramadhan na nilijua kama ni miongoni wa vijana machachari na hata mwaka huu wanawezekana wakaenda kutuwakilisha kule Misri katika ajenda ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mheshimiwa Spika, katika upande huo Serikali ni kama nilivyosema ni kwamba mwongozo huu uko katika hatua za mwisho, takriban mwezi mmoja uliopita tulikuwa katika kile kituo cha Carbon Tanzania ambacho sisi tumeki-center pale University of Sokoine Morogoro, tulikuwa na kikao hicho imani yetu ni kwamba mwanzoni mwa mwaka wa fedha unaokuja maana yake kuanzia Julai kwenda hapa mbele si muda mrefu mpango huo utaweza kukamili ili mradi kwamba watu waweze kushiriki katika ajenda hii kubwa ya kibiashara.

Name

Bakar Hamad Bakar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuomba fedha katika mifuko ya kupunguza hewa ukaa duniani na kuwalipa wananchi wanaopanda na kutunza misitu katika Wilaya ya Kilolo?

Supplementary Question 5

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana mimi nilitaja kujua tu kwamba je, Wizara hii ya Muungano na Mazingira ni kwa kiasi gani inashirikiana na Wizara ya Makamu wa Kwanza wa Rais ambayo pia nayo inashughulikia masuala ya mazingira katika kukabiliana na suala hili la changamoto ya gesi ukaa au hewa ukaa?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu kwamba Ofisi ya Makamu wa Rais ina deal na masuala ya Muungano Bara na Visiwani, Lakini masuala ya mazingira upande wa Zanzibar ni chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Hata hivyo tunafahamu kwamba ajenda ya mazingira ni ajenda mtambuka haina mipaka, ndiyo maana muda wote tumeweza kushirikiana vya kutosha kabisa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na ndiyo maana hata ukiangalia miradi mingine tunayoiandika katika bajeti yetu Madam Maryam pale Mbunge wa Pandani anafahamu kwamba katika jambo tulijadili katika kikao chetu katika Kamati yetu ya Bunge, miongoni mwa mambo jinsi gani miradi mbalimbali inaenda mpaka kule Zanzibar na hata hivyo ndiyo maana leo hii tuna miradi Kaskazini A, na hata mradi wa Sepwese pale tunaenda kujenga ukuta pale hii yote ni suala zima la mpango wa pamoja jinsi gani tunashughulika na ajenda ya mazingira katika maeneo yetu.

Name

Soud Mohammed Jumah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Donge

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuomba fedha katika mifuko ya kupunguza hewa ukaa duniani na kuwalipa wananchi wanaopanda na kutunza misitu katika Wilaya ya Kilolo?

Supplementary Question 6

MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mie kuuliza swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa misitu mingi ipo katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa; je, kuna utaratibu gani wa Serikali kuzihamasisha taasisi za Serikali kuweza kushiriki katika biashara hii ya hewa ukaa?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la kaka yangu Mheshimiwa Soud, mimi namuita encyclopedia ya mambo ya mazingira kwa sababu amebobea sana katika mambo ya mazingira katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni kwamba kama tulivyosema ni kwamba katika kushirikisha taasisi hizi hata sasa hivi ukiangalia kwa mfano TFS wana misitu mingi sana, lakini bado hawajanufaika katika hewa ya ukaa, ni halmashauri ya Katavi peke yake na kule kama tulivyosema Simanjiro ambao wao kwa mwaka ile own source collection katika hewa ya ukaa ni kubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ndiyo maana tumeweka mwongozo kwa lengo kubwa ni kwamba taasisi kwa mfano TFS, vijiji vyetu, halmashauri zetu na watu binafsi waweze kushiriki vizuri katika hewa ya ukaa. Kwa hiyo ndiyo jambo ambalo tuliona kulikuwa na gap hapo tunaenda kuya-address gap hii kwa lengo kubwa ni kwamba kujenga uchumi wa nchi yetu katika suala zima la hewa ya ukaa.