Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 8 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 116 2023-09-07

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka huduma ya mawasiliano ya simu katika maeneo ambayo orodha yake iliwasilishwa Wizarani – Urambo?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta, Mbunge wa Jimbo la Urambo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imetekeleza ujenzi wa minara kumi katika kata 10 ambazo ni kati ya kata 18 za Wilaya ya Urambo, ambapo minara tisa imekamilika katika Kata za Imalamakoye, Kasisi, Songambele, Itundu, Ukondamoyo, Nsenda, Uyogo, Vumilia, Ugalla pamoja na Uyumbu.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika baadhi ya Vijiji vya Kata ya Kasisi na Kiloleni na tayari imekwisha wapata watoa huduma wa kufikisha huduma ya mawasiliano katika kata hizo. Kwa upande wa kata za Kapilula, Kiyungi, Mchikichini na Muungano, Serikali kupitia UCSAF itafanya tathmini ili kupata hali halisi ya changamoto ya mawasiliano katika maeneo hayo.