Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 8 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 112 2023-09-07

Name

Michael Mwita Kembaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. MICHAEL M. KEMBAKI aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Shule ya Bweni ya Wasichana Tarime Mjini?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Michael Mwita Kembaki, Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 na 2022/2023, Serikali kupitia Mradi wa SEQUIP ilitoa shilingi bilioni 1.054 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili za Gicheri na Nyagisese zenye miundombinu yote ya madarasa, maabara, jengo la utawala na chumba cha kompyuta. Shule hizo zitakapokamilika zitaongezewa miundombinu ya mabweni ili ziweze kudahili wanafunzi wa kike.