Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 5 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 61 2023-09-04

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kuharakisha uwekaji samani kwenye maktaba na maabara Chuo cha FETA Mikindani?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Agnes Elias Hokororo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024 Serikali kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) inaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya kufundishia katika Kampasi zake ikiwemo ujenzi wa maabara na maktaba katika kampasi ya Mikindani. Pindi tuu ujenzi wa majengo hayo ya maktaba na maabara yatakapokamilika katika kampasi ya Mikindani, Serikali itaweka samani kwenye miundombinu hiyo muhimu. (Makofi)