Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 12 Sitting 4 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 50 2023-09-01

Name

Miraji Jumanne Mtaturu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mashariki

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Vituo vya Polisi kwenye Kata za Mkiwa, Misughaa na Mungaa pamoja na nyumba za kuishi askari Singida Mashariki?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Singida Mashariki, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inazo taarifa kuwa Kata za Mkiwa, Misughaa na Mungaa zimeshatenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Polisi na nyumba za makazi ya askari. Serikali kupitia Jeshi la Polisi inasubiri kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa vituo na nyumba hizo ili kuunga mkono kwenye ukamilishaji. Nakushukuru.