Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 11 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 144 2023-04-20

Name

Tamima Haji Abass

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza: -

Je, kuna utafiti uliofanywa na Serikali kujua sababu za uwepo wa Watoto wa mitaani?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wananwake na Makundi Maalum napenda kujibu swali la Mheshimiwa Tamima Haji Abass, Mbunge wa Viti Maalum) kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mwaka 2017/2018 ilifanya tafiti katika Mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Arusha na Iringa ili kubaini idadi na sababu za watoto kuishi na kufanya kazi mitaani ambapo walibainiwa jumla ya Watoto 6,393 (wavulana 4,865, wasichana 1,528). Vilevile, mwaka 2020/2021 Serikali ilirudia utafiti katika maeneo hayo na kubaini kuwa idadi ilipungua hadi watoto 4,383 (wavulana 3,508 wasichana 875).

Mheshimiwa Spika,miongoni mwa sababu zilizobainiwa ni pamoja na, malezi duni, yatima, migogoro kwenye familia, shinikizo la makundi rika, ukatili na unyanyasaji nyumbani, umasikini wa kipato katika familia na utumikishaji wa watoto mijini, ahsante.