Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 19 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 170 2022-05-10

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Daraja la Kalebe – Bukoba Vijijini ili kuwezesha magari yenye uzito zaidi ya tani kumi kupita kwenye daraja hilo?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi ya kujenga Daraja la Kalebe ambapo kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja hili inaendelea chini ya Mkataba wa Usanifu wa Barabara ya Kyaka II – Kanazi – Kyetema. Kazi ya usanifu imepangwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu wa 2022.

Mheshimiwa Spika, ahsante.