Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 16 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 130 2022-05-05

Name

Mariam Madalu Nyoka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA K.n.y. MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali ya Wilaya ya Songea?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mariamu Madalu Nyoka Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kati ya mwaka wa fedha 2019/2020 hadi 2021/2022 Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepokea Shilingi bilioni 3.1 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri. Jumla ya majengo 14 yamejengwa kwenye Hospitali hiyo ambapo majengo saba yamekamilika na majengo mengine saba ujenzi wake unaendelea katika hatua mbalimbali za ukamilishaji. Ahsante.