Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 17 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 148 2022-05-06

Name

Kasalali Emmanuel Mageni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumve

Primary Question

MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza: -

Je, ni lini barabara ya kilometa 73 kutoka Fulo – Nyambiti – Malya itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kasalali Emmanuel Mageni, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina barabara ya Fulo – Nyambiti – Malya yenye urefu wa kilometa 73 wakati wowote pindi fedha itakapopatikana. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kazi hii. Ahsante.