Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 17 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 142 2022-05-06

Name

Esther Edwin Maleko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: -

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza wataalam wa saikolojia kwenye jamii ili kutoa huduma za ushauri wa afya ya akili na namna ya kuondokana na msongo?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaona umuhimu na inathamini huduma ya msaada wa kisaikolojia na kijamii ambayo inatolewa na wataalam wa saikolojia kwa lengo la kukidhi mahitaji ya mtu kimwili, kihisia, kijamii, kiroho na kiakili katika mazingira anayoishi. Ahsante.