Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 15 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 124 2022-04-29

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mgambalenga Wilayani Kilolo?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo napenda kujibu swali la Mheshimiwa Justine Lazaro Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/ 2023, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu ya Mgambalenga yenye hekta 3,000 Wilayani Kilolo. Ujenzi huo utahusisha ukamilishaji wa mfereji mkuu wenye urefu wa kilometa 14 pamoja na maumbo yake.