Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 11 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 91 2022-04-22

Name

Elibariki Emmanuel Kingu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Magharibi

Primary Question

MHE. ELIBARIKI I. KINGU aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga majosho ya mifugo katika Kata za Makilawa, Igelansoni, Iyumbu, Ighombwe, Mgungira na Mwaru Wilayani Ikungi?

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Answer

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Elibariki Immanuel Kingu Mbunge wa Singida Magharibi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/ 2022, Wizara inakamilisha ujenzi wa majosho 168 katika Halmashauri 80 kwa gharama ya shilingi bilioni 3.033. Aidha, kati ya majosho hayo, majosho mawili yanajengwa katika Kata za Mgungira na Siuyu katika Halmashauri ya Ikungi.

Mheshimiwa Spika, Wizara inatambua uhitaji mkubwa wa majosho katika maeneo mbalimbali nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara itaendelea na ujenzi wa majosho katika maeneo yenye uhitaji yakiwemo ya Jimbo la Ikungi. Ahsante.