Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 9 Investment and Empowerment Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara 149 2023-02-10

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaziba nakisi ya uagizaji mafuta ya kula kwa kuruhusu uwekezaji mkubwa katika Bonde la Ziwa Tanganyika?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara napenda kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Jimbo la Mlalo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya mafuta ya kula nchini ikiwa ni pamoja na eneo la Bonde la Ziwa Tanganyika katika Mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa ili kukabiliana na uhaba uliopo. Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na uanzishwaji wa mashamba makubwa ikiwemo mashamba ya alizeti na michikichi, kuielekeza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) kuongeza utafiti na kuhamasisha sekta binafsi kuzalisha mbegu bora za mafuta katika mazao ya karanga, ufuta, alizeti na michikichi na kuhamasisha ushiriki wa taasisi za umma katika uzalishaji wa michikichi kwa ajili ya usindikaji wa mafuta ya kula katika Mkoa wa Kigoma.