Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 100 2023-02-07

Name

Iddi Kassim Iddi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. IDDI K. IDDI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga majosho ya kuogesha mifugo katika Halmashauri ya Msalala?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, (Mb), kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali ilifanya ukarabati wa majosho matano (5) katika kata za Burige, Lunguya, Mega, Ntobo na Ngaya zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala. Aidha, Serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majosho katika halmashauri mbalimbali nchini; ikiwemo Halmashauri ya Msalala. Pia Serikali inaendelea kuhamasisha wafugaji kuchangia ujenzi wa miundombinu ya mifugo ikiwemo ujenzi wa majosho. Ahsante.