Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 4 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 63 2023-02-03

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatatua migogoro ya Wakulima na Wafugaji Kata za Hembeti, Mkindo, Sungaji, Mtibwa, Kanga, Mziha na Doma?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi naomba kujibu swali Na. 63 la Mbunge wa Mvomero kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua uwepo wa migogoro ya wakulima na wafugaji katika Kata za Hembeti, Mkindo, Sungaji, Mtibwa, Kanga, Mziha na Doma Wilayani Mvomero. Kwa kutambua hilo, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo hatua ya mwaka 2013 ya kutenga kwa kutumia fedha za ndani kwenda kutatua migogoro katika jumla ya vijiji 72 kati ya vijiji 130 vilivyomo katika Wilaya hiyo ambavyo vimeandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi.