Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 4 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 59 2023-02-03

Name

Timotheo Paul Mnzava

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Vijijini

Primary Question

MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO K.n.y. MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia upatikanaji wa chakula cha bei nafuu kwa wananchi walioathirika na ukame nchini?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu Mheshimiwa Timotheo Paul Mnzava, Mbunge wa Korogwe Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeendelea kutoa chakula na kukiuza chini ya bei ya soko. Hadi kufikia tarehe 31 Januari, 2023, kiasi cha mahindi tani 24,975 zimepelekwa na kuuzwa katika Halmashauri 60 nchini katika vituo vya mauzo 116. Katika Halmashauri ya Korogwe, kituo cha mauzo kimefunguliwa eneo la Masewa tarehe 27 Januari, 2023. Jumla ya tani 32 zimepelekwa na tani 10 zimeshanunuliwa.