Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 4 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 49 2023-02-03

Name

Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa vijana walio mashuleni juu ya kujikinga na dawa za kulevya?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeandaa na kuzindua Mwongozo wa Utoaji Elimu Kuhusu Dawa za Kulevya nchini ambao ulizinduliwa tarehe 2 Julai, 2022 na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye kilele cha siku ya Taifa ya Kupinga Dawa za Kulevya, Jijini Dar es Salaam. Mwongozo huo tayari umeanza kutumika kuelimishia walimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na asasi za kiraia zinazojihusisha na utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo vijana waliopo mashuleni, juu ya tatizo la dawa za kulevya nchini.