Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 1 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 7 2023-01-31

Name

Bupe Nelson Mwakang'ata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga josho katika Kata ya Miula Wilayani Nkasi?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI aljibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Wizara ilipeleka kiasi cha shilingi milioni 108 kwa ajili ya ujenzi wa majosho sita katika Hamashauri ya Nkasi katika Vijiji vya Kipande, Katani, Chala, Mikukwe, Chalatila na Sintali. Majosho hayo yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kuwasiliana na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ili kukamilisha ujenzi wa majosho hayo na kutoa fursa kwa Serikali kutenga fedha zaidi kwa ajili ya ujenzi wa majosho mengine Nkasi Kusini ikiwemo Kata ya Miula. Aidha, Serikali inaendelea kuhamasisha wafugaji kuchangia ujenzi wa miundombinu ya mifugo ikiwemo majosho katika maeneo yao. Ahsante.