Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 8 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 122 2022-11-09

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA Nyangh’wale?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mbunge wa Jimbo la Nyangh’wale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inayo azma ya kujenga Chuo cha Ufundi Stadi katika kila Mkoa na Wilaya nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kujenga Vyuo vya VETA katika Wilaya 63 ambazo hazina vyuo hivyo. Kiasi hiki kitatumika pia katika ujenzi wa Chuo cha VETA katika Mkoa wa Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, Nyangh’wale ni miongoni mwa Wilaya 63 ambazo zipo kwenye mpango wa kujengewa Vyuo vya Ufundi Stadi kwa mwaka huu wa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.