Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 8 Foreign Affairs and International Cooperation Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 112 2022-11-09

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaajiri Maafisa Habari katika Balozi zetu ili kuutangaza nchi na vivutio mbalimbali?

Name

Amber. Mbarouk Nassor Mbarouk

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Felista Deogratius Njau, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa Maofisa wanaopelekwa Ubalozini, moja ya majukumu yao ya msingi ni kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje ambayo imeweka msisitizo katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi. Miongoni mwa majukumu ya kila Ofisa na kila Ubalozi ni pamoja na kutangaza vivutio vya utalii wetu, kubidhaisha Kiswahili, kuvutia wawekezaji na kutafuta fursa za masoko kwa bidhaa zetu. Aidha, Wizara ina utaratibu wa kuwajengea Watumishi uwezo kupitia mafunzo ili waweze kufanya kazi zaidi ya moja ikiwemo kuwa na uwezo wa kutoa habari muhimu kwa wadau.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.