Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 8 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 108 2022-11-09

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, nini mkakati wa Serikali kujenga chumba cha upasuaji kwa ajili ya Wajawazito katika Kituo cha Afya cha Itaka Wilayani Mbozi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 imepeleka shilingi milioni 300 kwenye Kituo cha Afya Itaka katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi. Fedha hizo zinatumika kujenga jengo la wazazi, na jengo la upasuaji. Ujenzi wa majengo hayo upo katika hatua ya msingi.