Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 93 2022-11-08

Name

Nicodemas Henry Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Skimu za Umwagiliaji katika Jimbo la Mbogwe?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na zoezi la utambuzi na uhakiki wa maeneo zaidi yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe. Hadi sasa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kushirikiana na wananchi wa Mbogwe wameweza kuibua Skimu ya Mugelele yenye eneo la ukubwa wa hekta 300. Aidha, baada ya zoezi hilo kukamilika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itatenga fedha katika bajeti ya mwaka 2023/2024 kwa ajili ya upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.