Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 10 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 154 2022-11-11

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MHE. NANCY H. NYALUSI K.n.y. MHE. DAVID M. KIHENZILE aliuliza: -

Je, lini skimu za umwagiliaji Ukanda wa joto Ihowanza, Malangali, Idunda, Mbalamaziwa, Itandulu, Nyololo na Maduma zitajengwa?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Mufindi Kusini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika Mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 itatenga fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa skimu za Ukanda wa joto za Ihowanza, Malagali Idunda, Mbalamaziwa, Itandu, Nyololo na Maduma. Baada ya kukamilisha zoezi hili Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa skimu hizo.