Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 78 2022-11-07

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: -

Je, kuna mkakati gani wa kuzuia nyavu haramu?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stella Simon Fiyao, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa Mkakati wa Kusimamia Rasilimali za Uvuvi ambao unajumuisha mbinu mbalimbali za kudhibiti utengenezaji, uagizaji, matumizi na biashara ya nyavu haramu za uvuvi. Utekelezaji wa mkakati huo unahusisha wadau mbalimbali ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama, sheria, watendaji wa taasisi zilizopo mipakani, bandarini na viwanja vya ndege; Viongozi wa Mikoa na Wilaya, wavuvi pamoja na watendaji wa Wizara kupitia vituo vya ulinzi wa rasilimali za uvuvi. Aidha, elimu kwa wadau kuhusu matumizi ya nyavu sahihi, uvuvi endelevu na wenye tija inaendelea kutolewa. Ahsante.