Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 4 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 61 2022-11-04

Name

Vincent Paul Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati wa Mahakama ya Mwanzo Chala?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Vincent Paul Mbogo, Mbunge wa Nkasi Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Tarafa ya Chala yenye Kata nne; za Chala, Nkadasi, Kipande na Mkwamba, ina Mahakama za mwanzo mbili za Chala na Kipande. Katika kuimarisha majengo ya Mahakama kwa kuzingatia mpango uliopo wa ujenzi na ukarabati wa Mahakama nchini, Mahakama ina mpango wa kukarabati jengo la Mahakama ya Mwanzo Chala katika mwaka wa fedha 2024/2025.