Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 3 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 40 2022-11-03

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza majengo katika Kituo cha Afya Itobo Wilayani Nzega?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jaqueline Kainja Andrea, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeshaanza kuongeza majengo katika Kituo cha Afya Itobo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nzega. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Shilingi milioni 500 zilipelekwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje, jengo la maabara, kichomea taka, jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji na jengo la kufulia nguo. Ujenzi wa majengo haya upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji. Ahsante.