Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 22 2022-11-02

Name

Jafari Chege Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Primary Question

MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza: -

Je, ni lini Mamlaka ya Mji Mdogo Shirati katika Wilaya ya Rorya itaanza kufanya kazi kama Mamlaka kamili?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Rorya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Shirati itaanza mara baada ya Halmashauri mama ya Rorya kukamilisha mchakato wake wa kukusanya na kuimarisha mapato ya ndani ili iweze kuzihudumia Halmashauri mama na Mamlaka ya Mji mdogo wa Shirati.