Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 1 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 13 2022-11-01

Name

Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: -

Je, ni kwa nini kusiwe na Mahakama ya Rufaa Tanzania Kanda ya Zanzibar badala ya kesi kusikilizwa kwa mwaka mara moja?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chumbuni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Rufaa Kanda ya Zanzibar ipo kwa sasa na inaendesha shughuli zake kupitia Masijala ndogo iliyopo Jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar. Hata hivyo, Serikali inaona umuhimu wa kuwa na jengo la Mahakama ya Rufani Zanzibar na inaendelea kulifanyia kazi.