Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 1 2022-11-01

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kumaliza barabara ya Manyinga hadi Madizini kwa kiwango cha lami?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jonas Van Zeeland Mbunge wa Jimbo la Mvomero, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilitenga fedha kiasi cha shilingi milioni 500.00 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa urefu wa kilomita 0.54 ambapo ujenzi huo umekamilika.

Mheshimiwa Spika, TARURA itaendelea na ukamilishaji wa kipande kilichobaki kulingana na upatikanaji wa fedha ili wananchi wa eneo la Madizini na sehemu zingine katika tarafa ya Turiani waweze kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi kwa ufanisi.