Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 3 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 41 2022-09-15

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya Kata ya Kagera/Nkanda Wilayani Kasulu?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 ilipeleka Shilingi Bilioni 1.4 kwenye Halmashauri ya Wilaya Kasulu kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya vya Kitanga, Nyenge na Rungwe Mpya. Ujenzi wa vituo hivi upo hatua mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2023/2024 itatenga fedha Shilingi Milioni 500 kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Kagera/Nkanda.