Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 108 2022-09-21

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza wataalam wa zao la zabibu Dodoma?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo napenda kujibu swali la Mheshimiwa Fatma Hassan Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imepata kibali cha kuajiri watumishi wapya 100 na wengine 68 kuhamia TARI kutoka Wizarani wakiwemo Maafisa Kilimo ambao watapelekwa katika vituo vya utafiti ikiwemo Kituo cha Uendelezaji wa Zao la Zabibu TARI Makutupora. Mkakati uliopo ni kuwajengea uwezo wa kutosha wataalamu waliopo kwa kuwapatia mafunzo mahsusi ya kilimo cha zabibu na kujifunza teknolojia mpya za kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa zao la zabibu.