Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 98 2022-09-21

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU K.n.y. MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafanya maboresho ya ujenzi na ukarabati Vituo vya Afya Chikobe na Bukoli ili vitoe huduma stahiki kwa wananchi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tumaini Bryceson Magessa, Mbunge wa Jimbo la Busanda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa mwaka 2023/2024 itatenga kutoka mapato ya ndani shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Kituo cha Afya cha Bukoli. Aidha katika mwaka huo, Halmashauri ya Wilaya ya Geita itatenga shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati katika Kituo cha Afya Chikobe. Ahsante.