Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 97 2022-09-21

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. JERRY W. SILAA K.n.y. MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: -

Je, ni lini Mradi wa Dar es Salaam Metrpolitan Development Project awamu ya pili utaanza katika Jimbo la Kigamboni?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na Benki ya Dunia juu ya mkopo wa fedha kwa ajili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP) ambapo Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitanufaika pamoja na Jimbo la Kigamboni. Aidha, maandalizi ya mradi huo yanategemewa kuanza mwezi Januari, 2023.