Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 8 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 132 2022-09-22

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: -

Je, kwa takwimu ni wahitimu wangapi wa kada ya Ualimu wa masomo ya sayansi na hesabu hawajaajiriwa tangu mwaka 2015?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Esther Nicholaus Matiko, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2015 hadi 2022 jumla ya wahitimu 33,492 wa kada ya Ualimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati wamehitimu mafunzo katika Vyuo mbalimbali vya Ualimu na Vyuo Vikuu. Kati yao wahitimu 13,383 wameajiriwa katika shule mbalimbali nchini tangu mwaka 2015. Aidha, wahitimu 20,109 hawajaajiriwa katika shule za Serikali.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuajiri ili kukidhi mahitaji ya Walimu katika shule za umma. Nakushukuru sana.