Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 1 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 13 2022-09-13

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itarejesha utoaji wa ruzuku ya pembejeo za dawa kwa wakulima wa kahawa?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo napenda kujibu swali la Mheshimiwa Profesa Patrick Alois Ndakidemi, Mbunge wa Moshi Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kutokana na kukua kwa teknolojia ambako kumewezesha kugunduliwa kwa miche chotara ya kahawa ambayo ina ukinzani na magonjwa makuu ya kahawa ya kutu ya majani na Chole Buni, Serikali inaendelea kutekeleza mkakati wa kuzalisha miche bora ya kahawa milioni 20 yenye ukinzani mkubwa wa magonjwa na ambayo hutolewa kwa ruzuku kupitia Taasisi ya Utafiti TaCRI na Bodi ya Kahawa Tanzania.