Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 2 2022-09-13

Name

Salim Alaudin Hasham

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulanga

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA K.n.y. MHE. ALAUDIN H. SALIM aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali mpya ya Wilaya ya Ulanga?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alaudin Hasham Salim, Mbunge wa Jimbo la Ulanga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga ina Hospitali ya Wilaya Ulanga ambayo ni kongwe na chakavu. Serikali itafanya tathmini ya hospitali hiyo ili kufanya maamuzi ya kuikarabati katika bajeti ya mwaka 2023/2024 au kuweka mpango wa kujenga hospitali mpya. Ahsante.