Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 1 2022-09-13

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga Shilingi bilioni 16.55 kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa wa hospitali kongwe za Halmashauri 19 kote nchini. Hospitali ya Halmashauri ya Mpwapwa ni miongoni mwa Hospitali hizo ambapo imetengewa Shilingi milioni 900 kwa ajili ya kazi hiyo. Ahsante.