Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 6 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 160 2022-02-18

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizo la upungufu wa wataalamu wa afya hasa ma-nurse katika Vituo vya Afya na Zahanati Mkoani Morogoro?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali iliajiri watumishi 2,726 wa kada mbalimbali za afya na kuwapeleka kwenye Halmashauri zote 184 ambapo Mkoa wa Morogoro ulipata jumla ya watumishi 156 ambao walipelekwa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali ni kuendelea kuajiri wataalam wa afya na kuwapeleka vituoni nchini kote. Ahsante.