Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 6 Sitting 12 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 134 2022-02-16

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Primary Question

MHE. REUBEN N. KWAGILWA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga miundombinu ya kisasa katika mnada wa Nderema?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilwa, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi 287,194,890 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi na uboreshaji wa miundombinu katika mnada wa mifugo wa Nderema uliyopo Halmashauri ya Mji wa Handeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mzabuni ameshapatikana na ameshakabidhiwa mradi mwezi Januari, 2022 na sasa ujenzi umeshaanza. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2022 kwa mujibu wa mkataba.