Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 6 Sitting 10 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 119 2022-02-14

Name

Francis Isack Mtinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali italirejesha Shamba la kupumzishia Mifugo la Kinyangiri kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Francis Isack Mtinga, Mbunge wa Iramba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia umuhimu wa maeneo haya katika biashara ya mifugo na mazao yake, hususan kipindi hiki ambapo soko la nyama limezidi kuongezeka nje ya nchi, Serikali inakusudia kuendelea kuboresha maeneo yake yote ya mifugo ikiwa ni pamoja na eneo la Kinyangili ili kusudi biashara ya mifugo na biashara ya nyama nchini iweze kushamiri kwa kuzingatia viwango vyote vinavyotakiwa katika Soko la Kitaifa na Kimataifa. Ahsante. (Makofi)