Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 6 Sitting 10 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 118 2022-02-14

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. DEUS C. SANGU aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga mialo katika Forodha za Nankanga na Ilanga zilizopo ndani ya Ziwa Rukwa ili kurahisisha shughuli za Uvuvi?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango mkakati wa Serikali ni kuhakikisha inajenga na kuboresha mialo katika maeneo mbalimbali nchini yanayojishughulisha na shughuli za uvuvi ikiwemo maeneo yanayozunguka Ziwa Rukwa kama vile forodha za Nankanga na Forodha ya Ilanga. Aidha, utekelezaji wa mkakati huu unategemea upatikanaji wa rasilimali fedha.